Sunday, March 10, 2019

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 11.03.2019: Guardiola, Gundogan, Jokanovic, Mbappe

Pep GuardiolaPep Guardiola, ambaye hivi karibuni alihusishwa na Juventus, amewaambia marafiki zake kuwa yuko tayari kusalia Manchester City kwa miaka minne ijayo. (Telegraph)
Guardiola ametilia shaka hatima ya kiungo wa kati, Ilkay Gundogan katika klabu ya Manchester City baada kufichua kuwa mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 28 huenda usiongezwe. (Mirror)
West Brom itafanya mazungumzo zaidi na meneja wa zamani wa Fulham, Slavisa Jokanovic siku ya Jumatatu wanapoendelea na kampeini ya kumsaka kocha mpya baada ya Darren Moore kufutwa kazi. (Telegraph)
Tottenham na Arsenal huenda wakamshindania kiungo wa kati wa na Villarreal, Pablo Fornals, 23.
Celtic inapania kumsaini mlinzi wa Chelsea, Tomas Kalas, 25, amabye anachezea Bristol City kwa mkopo. (Daily Record)
Kilmarnock imetoa ofa ya awali kabla ya kuingia mkataba na kiungo wao wa kati wa zamani, Craig Bryson, 32, wa Derby ambaye mkataba wake unakamilika mwisho wa msimu huu. (Express)
Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amemkosoa Eden Hazard kwa kutocheza vizuri licha ya kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Wolves. (Talksport)
chanzo   BBC

No comments:

Post a Comment