Hakuna hata mtu mmoja aliyenusurika kati ya watu 157 waliokuwa kwenye ndege ya shirika la ndege la Ethiopia iliyoanguka leo asubuhi ikitokea mji mkuu wa Ethiopia Adis Ababa kuelekea Nairobi Kenya.
Raia kutoka mataifa 33 walikuwemo kwenye ndege hiyo yenye nambari ya usajili ET 302 iliyoanguka karibu na mji wa Bishoftu ulioko kiasi kilomita 50 Kusini Mashariki mwa mji mkuu Addis Ababa kwa mujibu wa ripoti.
Msemaji wa shirika la ndege ya Ethiopia ameliambia shirika la habari la kijerumani Dpa, kwamba raia 32 wakenya, Waethiopia 17, na wachina 8 ni miongoni mwa abiria waliokufa waliokuwa wakisafiri na ndege hiyo. Wamo pia raia kutoka mataifa ya Ufaransa, Italia, Canada, Marekani, Uingereza, Slovakia, Uholanzi, Misri na India.
Ndege aina ya Boeing 737 iliyokuwa na abiria 149 na wafanyakazi 8 iliruka mwendo wa saa 8.38 za asubuhi kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole na kupoteza mawasiliano dakika chache baadae kwa mujibu wa shirika hilo la ndege la Ethiopia. Ofisi ya waziri mkuu wa Ethiopia kwa niaba ya serikali imetowa ujumbe wa salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo.
Shughuli ya utafutaji miili na uokoaji zinaendelea ingawa imeelezwa kwamba rubani wa ndege hiyo alikabiliana na hitilafu na kutoa taarifa na kisha kuelekezwa kurudi mjini Adis Ababa kwa mujibu wa shirika la ndege.
ODDO NEWS
Sunday, March 10, 2019
YANGA HII MOTO CHINI, YAKOMBA POINTI ZOTE TATU KWA MKAPA

YANGA wanadhidhirisha kwamba ukubwa dawa kwani licha ya kufungwa mapema dakika ya 16 na mshambuliaji wa KMC, Rashid Mohamed walinyanyuka na kuendeleza moto wao kwenye ligi kwa kuwatungua mabao 2-1 wapinzani hao mchezo uliochezwa leo Uwanja wa Taifa.
Bao la Yanga lilipachikwa na Papy Tshishimbi dakika ya 37 baada ya Deus Kaseke kupiga kona fupi iliyotua miguuni mwa Deus Kaseke kabla ya kupiga pasi iliyomkuta Tshishimbi na kufunga bao safi la kichwa.
Mpaka mapumziko timu zote zilikuwa zimetoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 hali iliyowafanya KMC waamini kwamba watarejea na pointi moja kutoka kwa vinara wa ligi kwa sasa Yanga ambao wana pointi 70.
KMC waliongeza moto wa mashambulizi kipindi cha pili ambapo kocha wa KMC Ettiene Ndirayagije alianza kwa mabadiliko kwa kumtoa mlinda mlango Jonathan Nahimana nafasi yake ikachukuliwa na Juma Kaseja.
Dakika ya 62 Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera alifanya mabadiliko ya kiufundi kwa kumtoa Deus Kaseka akaingia Ibrahim Ajibu na Thaban Kamusoko nafasi yake ikachukuliwa na Amiss Tambwe.
Mabadiliko hayo yalileta matokokeo chanya kwani dakika ya 67 Ibrahim Ajibu alipiga pasi moja kumtamfuta Tambwe iliyomaliziwa na beki wa KMC Ally Ally ambaye alijifunga kwa kichwa safi kilichomshinda Kaseja wakati akiokoa mpira.
Baada ya bao hilo Kaseja alinyanyuka kishujaa na kumnyanyua All Ally ambaye alikuwa amekata tamaa baada ya kufunga bao lililodumu mpaka dakika 90 zinakamilika.
Timu ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Fanikiwa stars imeibuka na ushindi mzito wa mabao manne kwa mawili (4-2) dhidi ya timu ya chuo cha mawasiliano na kompyuta Kiitec unitedkatika uwanja wa chuo hicho uliopo maeneo ya Moshono jijini Arusha.
Timu ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Fanikiwa stars imeibuka na ushindi mzito wa mabao manne kwa mawili (4-2) dhidi ya timu ya chuo cha mawasiliano na kompyuta Kiitec unitedkatika uwanja wa chuo hicho uliopo maeneo ya Moshono jijini Arusha.
Mchezo huo wa kirafiki uliozikutanisha timu hizo kwa mara ya kwanza kihistoria siku ya Ijumaa ya tarehe 08 February 2019, katika dimba hilo la Moshono na kuudhuriwa na mamia ya mashabiki wa timu zote mbili huku wengi wao wakiwa ni wanafunzi kutoka katika vyuo hivyo.
Mchezo ulianza kwa kasi ya aina yake huku Fanikiwa Stars wakiongoza kwa kulishambulia kwa kasi lango la timu ya Kiitek United na baada ya dakika chache tu baada ya mpira kuanza, mchezaji wa Fanikiwa Stars alichezewa rafu katika eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo Patrick Tembaakaamuru penati ipigwe na Fanikiwa Stars kuandika bao la kwanza, hadi kipindi cha kwanza kuisha Fanikiwa Stars walikua wakiongoza kwa ushindi wa bao 2-0.

Baada ya mapumziko Kiitek United walikuja kwa kasi wakilisakama lango la Fanikiwa Stars kwa kutafuta nafasi ya kusawazisha, na hatimae dakika ya 54 nahodha wa timu hiyo alipiga mpira wa kutenga uliokwenda moja kwa moja katika lango la Fanikiwa Stars na kuiandikia timu yake bao la kwanza la kusawazisha.
Hadi dakika tisini za mwamuzi wa mchezo huo zinamalizika Fanikiwa Stars walikua wakuongoza kwa magoli manne kwa mawili ya Kiitec United ya Moshono jijini Arusha.
Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 11.03.2019: Guardiola, Gundogan, Jokanovic, Mbappe
Pep Guardiola, ambaye hivi karibuni alihusishwa na Juventus, amewaambia marafiki zake kuwa yuko tayari kusalia Manchester City kwa miaka minne ijayo. (Telegraph)
Guardiola ametilia shaka hatima ya kiungo wa kati, Ilkay Gundogan katika klabu ya Manchester City baada kufichua kuwa mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 28 huenda usiongezwe. (Mirror)
West Brom itafanya mazungumzo zaidi na meneja wa zamani wa Fulham, Slavisa Jokanovic siku ya Jumatatu wanapoendelea na kampeini ya kumsaka kocha mpya baada ya Darren Moore kufutwa kazi. (Telegraph)
Tottenham na Arsenal huenda wakamshindania kiungo wa kati wa na Villarreal, Pablo Fornals, 23.
Celtic inapania kumsaini mlinzi wa Chelsea, Tomas Kalas, 25, amabye anachezea Bristol City kwa mkopo. (Daily Record)
Kilmarnock imetoa ofa ya awali kabla ya kuingia mkataba na kiungo wao wa kati wa zamani, Craig Bryson, 32, wa Derby ambaye mkataba wake unakamilika mwisho wa msimu huu. (Express)
Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amemkosoa Eden Hazard kwa kutocheza vizuri licha ya kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Wolves. (Talksport)
chanzo BBC
Saturday, March 9, 2019
Picha za satellite zinaashiria kuwa Korea Kaskazini inajiandaa 'kurusha' kombora

Picha za Satellite kutoka kituo kimoja karibu na mji wa Pyongyang zinashiria kuwa Korea Kaskazini inajiandaa 'kurusha kombora' ama roketi.
Kumeripotiwa shughuli nyingi katika eneo linalofahamika kama Sanumdong, ambapo Korea Kaskazini huunganishia makombora na maroketi yake.
Mapema wiki hii ripoti ziliibuka kuwa Korea Kaskazini imejenga kituo kikuu cha kikuu cha kuundia silaha zake za nuklia.
Shughuli ya kubomoa kituo cha Sohae ilianza mwaka jana lakini ikasitishwa baada ya mazungumzo kati ya marais Kim Jong un na Donald Trump kuvunjika.
Siku ya Ijumaa rais Trump alisema atasikitika sana ikiwa Korea Kaskazini itarejelea tena kufanyia majaribio silaha zake hatari.

Magari makubwa yameonekana yakizunguka kituo cha silaha cha Sanumdong, hali ambayo siku zilizopita ziliashiriria kuwa Korea Kaskazini ilikuwa ikijiandaa kufyetua Kombora ama roketi kutoka eneo hilo.
Picha za satellite zimechapishwa na mitambo maalum ya Marekani inayofahamika kama NPR.
Mwandishi wa BBC mjini correspondent Laura Bicker amesema Korea Kaskazini huenda akaamua kuchukua hatua hiyo baada ya mazungumzo ya Hanoi kati ya Donald Trump na Kim Jong-un kumalizika bila kufikia muafaka wowote.
Ameongeza kuwa wataalamu wanahofia mitambo inayotumiwa kurusha silaha hizo hatari sio hasa kwa makombora ya masafa marefu.
Kulikuwa na matumaini kuwa viongozi hao wangelifikia mkataba wa kumaliza mzozo kati yao japo Korea Kaskazini ilikuwa tayari kupunguza shughuli zake za nuklia ikiwa Marekani ingeliondolea baadhi ya vikwazo dhidi yake.
Kituo cha kurusha makombora cha Sohae Tongchang-ri kimetumiwa kufanyia majaribio majaribio baadhi ya silaha zake lakini siyo makombora ya masafa marefu.
Wiki hii picha za satellite, kutoka vituo kadhaa vya Marekani na pamoja na ushahidi kutoka shirika la kijasusi la Korea Kusini, zilionesha ujenzi upya katika mitambo ya kurusha maroketi.
source BBC.
Subscribe to:
Comments (Atom)